Kilimo cha tufaha ni mradi wenye faida kubwa. Mahitaji ya matunda yanazidi kudaiwa na wateja.
Ili kupanda mtufaha, chimba shimo la futi 2–3 kwa kina na upana. Changanya udongo na mbolea oza kabla ya kupandikiza miche. Mwagilia miche baada ya kupandikiza. Mara tu mti umeota umwagilie maji mara moja kwa wiki. Usipande mazao kama mahindi, mtama katika bustani ya mitufaha kwani yatashindana na mitufaha. Usipande nyanya pia kwani zinaweza kupanda mitufaha. Kumwagilia shamba wakati wa kiangazi husaidia kuboresha uzalishaji.
Faida za tufaha
Mazao yanaweza kuuzwa kwa soko la ndani na nje ya nchi, jambo ambalo huwahimiza wakulima na wateja kutumia tufaha zilizozalishwa nchini. Pia ni chanzo cha azira, na hivyo husaidia kuondoa umaskini.