Kaya nyingi nchini Uganda hufuga kuku wa kienyeji kwenye mfumo wa ufugaji huria. Katika usimamizi mzuri, tija inaweza kuongezeka.
Katika ufugaji huria, ndege wanaruhusiwa kutembea ndani ya eneo pana ambalo linaweza kuzungushiwa na uzio. Katika wakati wa usiku, kuku huhifadhiwa ndani ya banda. Ukubwa wa kundi la kuku hutofautiana kulingana na uwezo wa kifedha, vifaa, mitizamo na vipaumbele vya mfugaji. Ili kulinda mazao kutoharibiwa na kuku wakati wa msimu wa upandaji, kuku huhifadhiwa katika mabanda, jambo ambalo husababisha upungufu wa lishe kwa ndege.
Kulisha kuku
Ulishaji wa ndege kwa njia huria huathiriwa na upatikanaji wa chakula asili, pamoja na msimu. Hali ya hewa ya joto na kavu huhimiza ukuaji wa wadudu wengi, wakati hali ya hewa baridi huhimiza uzalishaji wa minyoo zaidi.
Kuruhusu ndege kuingia katika zizi la ng‘ombe kunaweza kuruhusu ndege kupata malisho kama vile kupe na minyoo. Eneo la kufugia kuku kwa njia huria linaweza kupanuliwa kwa kutumia maeneo yaliyo chini ya miti hasa chini ya bustani.
Ndege wanaofugwa kwa njia huria pia wanaweza kupewa chakula cha nyongeza na chakula kinachotengenezwa kama vile samaki, soya na karanga zilizosagwa, na minyoo.
Tabia mbaya katika kuku
Mimea ambayo ni chakula kikuu cha kuku wanaofugwa kwa njia huria ina madini kidogo. Hii ndiyo maana kuku hudonoa manyoya, pamoja na kujila wenyewe .
Upungufu wa protini unahusishwa na udonoaji wa manyoya. Kwa ujumla, udonoaji wa manyoya hupungua kadri viwango vya fumuele katika lishe vinavyoongezeka.