Katika ufugaji wa kuku wa nyama, kutotolesha vifaranga na kulisha ni changamoto kubwa. Mbinu bora katika ufugaji wa kuku husaidia kuongeza tija ya biashara.
Katika usimamizi wa vifaranga, uingizaji wa hewa ni muhimu sana. Tunahitaji kutolea ndege halijoto sahihi na kuondoa hewa mbaya kwa mfano kabonidioksidi, amonia na kabonimonoksidi kutoka kwa banda la kuku. Huku kunatekelezwa kwa kuinua au kushusha mapazia kulingana na hali iliyopo.
Kushughulikia mapazia
Mapazia kwenye eneo la kutotoleshea vifaranga huinuliwa au hushushwa kulingana na tabia za vifaranga na usomaji wa kipima joto. Wakati wa joto, inua pazia ili kuingiza hewa, na wakati wa baridi, inua pazia huku ukiacha nafasi ya takriban sm 15 ili kuruhusu hewa safi kuingia ndani ya banda. Ni makosa kuongeza uingizaji wa hewa kwa kuinua pazia kutoka chini kwenda juu kabisa kwa sababu huku kunaweza kuondoa joto lililokusanywa.
Mkusanyiko wa gesi ya amonia kwenye banda la kuku husababisha harufu mbaya, kuwashwa kwa macho ya kuku, na kuathiri mfumo wao wa kupumua.
Kulisha ndege
Kuanzia siku ya 1 hadi 14, lisha ndege kwa chakula cha kuanzia ambacho kina asilimia 21% ya protini. Chakula hiki kina lishe na husaidia katika ukuaji wa ndege. Kuanzia siku ya 14 hadi 21, lisha ndege wako kwa chakula cha ndege wanaokua. Kutoka siku ya 21 hadi 28 lisha ndege kwenye chakula cha kumalizia. Ni muhimu huruhusu ndege wako kupumzika. Watolee giza ili wapumzike na kusaga chakula.
Kwa siku 5 za kwanza, changanya dawa ya mfadhaiko katika maji ya ndege ili kupunguza mfadhaiko. Hakikisha ndege daima wana maji bora ya kunywa wakati wote.
Kagua shingo ya vifaranga ili kuhisi kama wamelishwa au wamenyweshwa. Ikiwa sehemu hiyo ngumu, jua kwamba kifaranga amekula tu, ikiwa nyororo sana basi kifaranga amekunywa maji tu, na ikiwa inahisi kama uji uji, basi kifaranga amekunywa na kula.