»Mpango wa kibiashara wa ufugaji wa mbuzi«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=W1x2BRLGd6w

Muda: 

00:04:36
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

Business Ideas English

Kwa kuwa ni biashara yenye faida kubwa, ubora na wingi wa bidhaa zinazopatikana kwa ufugaji wa mbuzi hubainishwa na mbinu ya uzalishaji inayotumika.

Ufugaji wa mbuzi ni biashara yenye faida na huchangia lishe ya wafugaji na kuwatolea kipato. Mbuzi hutunzwa kwa urahisi. Usimamizi wa mbuzi hauhitaji vifaa vingi, mtaji mwingi au vibarua vingi.

Usimamizi wa mbuzi

Kwa usimamizi mzuri, tengeneza mpango mzuri wa biashara ya ufugaji mbuzi. Chagua eneo linalofaa ambalo lina vifaa vinavyohitajika kwa ufugaji wa mbuzi ambavyo ni pamoja na maeneo yenye maji bora, vyanzo vya chakula, shamba lenye rutuba kwa ukuaji mzuri wa nyasi. Kulisha mbuzi malisho ya kijani hupunguza gharama za chakula na huwafanya wanyama kuwa na tija.

Vile vile, lazima kuwe na vibarua wa kudumu, usafirishaji bora na huduma za daktari wa mifugo. Pai jenga banda la mbuzi mahali palipo inuliwa ambapo maji ya mvua hayatatwama, na banda lazima liingize mwanga wa kutosha.

Sakafu ya banda lazima inuliwe futi 4–5 kutoka ardhini na paa liwe futi 6–8 kutoka kwa sakafu. Sakafu ya banda inapaswa kujengwa kwa mbao huku nafasi zikiachwa kati yazo ili kuruhusu mkojo na kinyesi kuanguka chini. Ili kulinda mbuzi dhidi ya kibaridi, weka damani za plastiki kwenye nyavu za madirisha.

Usimamizi mzuri wa malisho ya mbuzi ni muhimu kwa ufugaji wa kibiashara, kwani kwa kawaida mbuzi hula nyasi, vitamini na maji kwa ukuaji mzuri. Unahitaji ujuzi wa kutosha kuhusu ulishaji wa mbuzi, na usiwalishe chakula kilichochafuliwa au maji machafu, na pia safisha banda kila mara.

Tenganisha wanambuzi na tunza mbuzi wa kuzaliana na wajawazito. Ruhusu wanambuzi wawe na mama yao kwa wiki kadhaa baada ya kuzaliwa. Uhimilishaji bandia ni njia nzuri ya kuzaliana.

Chanja mbuzi kwa wakati, na dumisha uhusiano mzuri na daktari wa mifugo.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:13Ufugaji wa mbuzi ni biashara yenye faida na huchangia lishe ya wafugaji.
00:1400:28Mbuzi hutoa kipato kwa wafugaji na hutunzwa kwa urahisi.
00:2900:59Kwa usimamizi mzuri, tengeneza mpango mzuri wa biashara ya ufugaji mbuzi
01:0001:36Chagua eneo linalofaa ambalo lina vifaa vinavyohitajika kwa ufugaji wa mbuzi.
01:3701:42Kulisha mbuzi malisho ya kijani hupunguza gharama.
01:4301:51Lazima kuwe na vibarua wa kudumu, usafirishaji bora na huduma za daktari wa mifugo
01:5202:01Pai jenga banda la mbuzi mahali ambapo maji ya mvua hayatatwama
02:0202:05Banda lazima liingize mwanga wa kutosha.
02:0602:22Sakafu ya banda lazima inuliwe futi 4–5 kutoka ardhini na paa liwe futi 6–8 kutoka kwa sakafu.
02:2302:31Sakafu ya banda inapaswa kujengwa kwa mbao huku nafasi zikiachwa kati yazo
02:3202:40Weka damani za plastiki kwenye nyavu za madirisha.
02:4103:04Unahitaji ujuzi wa kutosha kuhusu ulishaji wa mbuzi.
03:0503:16Usipe mbuzi maji machafu na chakula kilichochafuliwa
03:1703:27Tenganisha wanambuzi na tunza mbuzi wa kuzaliana na wajawazito
03:2803:31Ruhusu wanambuzi wawe na mama yao kwa wiki kadhaa baada ya kuzaliwa.
03:3203:42Uhimilishaji bandia ni njia nzuri ya kuzaliana.
03:4303:58Chanja mbuzi kwa wakati, na dumisha uhusiano mzuri na daktari wa mifugo.
03:5904:34Magonjwa ni hatari kwa mbuzi.
04:3504:36Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *