»Mpango wa kibiashara wa shamba la bata –Ufugaji wa bata weupe«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=ElIb7hhkJqs

Muda: 

00:04:11
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

Business Ideas English

Kwa kuwa ni biashara yenye faida kubwa, ubora na wingi wa bidhaa zinazopatikana kwa ufugaji wa bata hubainishwa na mbinu ya uzalishaji inayotumika.

Nyama ya bata ni ladha na ina wateja wengi sana. Katika miezi 3, bata dume huwa na uzito wa kilo 5. Ufugaji wa bata huhitaji nafasi ndogo na ni biashara yenye faida kubwa.

Usimamizi wa bata

Kwa usimamizi mzuri wa ufugaji wa bata, banda linapaswa kuwekwa katika maeneo iliyokaribu na maji ya kutosha. Kila bata huhitaji nafasi ya futi 4–5 za mraba. Vifaranga vya umri wa siku moja vinafaa kutunzwa ipaswavyo katika mahali maalum palipo na halijoto ya nyuzi joto 95 katika wiki ya kwanza. Punguza halijoto kwa nyuzi joto 5 kila wiki, na vifaranga hutunzwa katika eneo hilo kwa wiki 3–4 katika msimu wa kiangazi, na wiki 6–7 katika msimu wa baridi.

Vile vile, banda la vifaranga linapaswa kujengwe katika sehemu ambazo hazina unyevu. katika hili, tandaza pumba kavu za mpunga au pumba za mbao kwenye sakafu. Baada ya kuhesabu vifaranga, wape maji yaliyochanganywa na vitamini. Lisha kila kifaranga gramu 5 kila siku.

Kulisha bata kwa malisho bora ni muhimu, na malisho haya yanaweza kuwa ya asili, yaliyotengenezwa tayari au chakula cha kuku. Usiwape bata chakula kikavu, hivyo basi wape maji na chakula cha unga, na ulishe bata kwa muda wa wiki 6. Ili kufanikiwa na kuzaliana, hifadhi bata dume 1 kwa majike 5–9, na uwatolee chanzo cha maji.

Bata huathiriwa na kipindupindu. Wanaweza kuuzwa kwa miezi 3, na kiwango cha vifo ni kidogo sana. Bata huchanjwa ndani ya siku 25 na pia baada ya siku 40.

Bidhaa za bata zina wateja wengi sana. Anzisha mikakati uuzaji sokoni kabla ya kuanza kufuga bata.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:15Nyama ya bata ni ladha na ina wateja wengi sana.
00:1600:37Katika miezi 3, bata dume huwa na uzito wa kilo 5. Ufugaji wa bata huhitaji nafasi ndogo
00:3800:47Ufugaji wa bata ni biashara yenye faida kubwa ikiwa umetekelezwa vizuri.
00:4800:59Banda linapaswa kuwekwa katika maeneo iliyokaribu na maji ya kutosha
01:0001:17Kila bata huhitaji nafasi ya futi 4–5 za mraba.
01:1801:25Vifaranga vya umri wa siku moja vinafaa kutunzwa ipaswavyo katika mahali maalum
01:2601:36Punguza halijoto kwa nyuzi joto 5 kila wiki
01:3701:52Jenga banda la vifaranga katika maeneo ambayo hayanaunyevu
01:5301:58Tandaza pumba kavu za mpunga au pumba za mbao kwenye sakafu
01:5902:16Baada ya kuhesabu vifaranga, wape maji yaliyochanganywa na vitamini.
02:1702:56Lisha kila kifaranga gramu 5 kila siku
02:5703:06Usiwape bata chakula kikavu, hivyo basi wape maji na chakula cha unga.
03:0703:24Lisha bata kwa muda wa wiki 6. Ili kufanikiwa na kuzaliana, hifadhi bata dume 1 kwa majike 5–9
03:2503:32Bata huathiriwa na kipindupindu.
03:3303:41Wanaweza kuuzwa kwa miezi 3, na kiwango cha vifo ni kidogo sana.
03:4203:52Bata huchanjwa ndani ya siku 25 na pia baada ya siku 40.
03:5304:04Bidhaa za bata zina wateja wengi sana
04:0504:09Anzisha mikakati uuzaji sokoni kabla ya kuanza kufuga bata.
04:1004:11Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *