Karantini ni mahali ambapo wanyama hutenganishwa na kundi zima ili kuhakikisha afya ya mifugo.
Eneo la karantini ni lazima liwe shambani. Linaweza kusaidia kutenganisha wanyama watakaochanjwa, wanyama watakaopokea matibabu pamoja na kutenganisha kundi jipya kutoka kwa kundi zee. Unaponunua mifugo sokoni, usiwachanganye na kundi lako kwa sababu mara nyingi, hawa ni wanyama kutoka kwenye mashamba duni ambayo yanaweza kusababisha matatizo kama vile magonjwa wakichanganywa na kundi lako.
Kushughulikia mbuzi wapya
Iwapo unaleta kundi la kwanza la wanyama, usiwaweke karantini kwa sababu wote ni wapya na zizi lao ni karantini yenyewe, lakini ikiwa utaleta kundi lingine, basi lazima uwatenganishe.
Wanyama wanapohamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine, kingamwili zao hupungua na ikiwa mnyama ana ugonjwa wowote, ugonjwa huo huibuka kwa urahisi kutokana na kingamwili iliyopungua. Katika karantini, unahifadhi wanyama wako pamoja na kuwachunguza kwa angalau wiki 1. Ikiwa mnyama ana dalili zozote za ugonjwa, mtibu na pia mpe vitamini nyingi ili kuongeza kingamwili yake.
Sababu ya kutenganisha au kuweka mifugo karantini
Karantini inaweza kutumika kushughulikia mifugo mpya, kufuatilia wanyama wanaoshukiwa kuwa wagonjwa kwa urahisi, na wale na wale ambao hawafanyi vizuri, na kuruhusu wanyama wazoeane kabla ya kuwaweka zizini.