wa kuwa ni mojawapo ya mambo yanayoathiri ufugaji wa wanyama, afya ya mnyama huamua ubora na wingi wa bidhaa zinazopatikana.
Ugonjwa wa homa ya mapafu (Bovine Respiratory) ndio chanzo kikuu cha vifo vya ndama walio na umri wa zaidi ya wiki tatu, na ni ugonjwa ghali zaidi ambao hufanya ufugaji wa wanyama kuwa na changamoto.
Udhibiti wa magonjwa
Viini vya mannheimia haemolytica huingia puani mwa ndama mara tu baada ya kuzaliwa. Viini hivyo husababisha maambukizi ambayo huathiri sehemu za juu za kupumua. Viini huendela huvamia mapafu ya mnyama na kuongezeka idadi. Hii huchochea vijidudu muhimu kusafiri hadi kwenye mapafu ili kuvamia viini.
Vile vile, viini vya mannheimia haemolytica huzalisha sumu ambayo huharibu na kuua vijidudu muhimu. Mara baada ya vijidudu muhimu kuharibiwa, huzalisha vimeng‘enya ambavyo husababisha uharibifu na ugonjwa wa mapafu.
Bakteria hawa hawana kiini kinachochochea utengenezaji wa kingamwili ambazo hupunguza sumu, na kwa hivyo bakteria hawawezi kumlinda mnyama dhidi ya uharibifu unaosababishwa na sumu. Chanjo aina ya Presponse SQ ina bakteria zote mbili za kingamwili ambazo huzuia uharibifu unaosababishwa na sumu, jambo ambalo huruhusu vijidudu muhimu kuua viini vya mannheimia haemolytica, na hivyo kupunguza uharibifu wa mapafu.
Hatimaye chagua chanjo zinazoaminika ambazo husaidia kulinda ng‘ombe dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu.