Mbaazi hukabiliwa na uharibifu unaosababishwa na mabuu ya wadudu. Uharibifu huu unaweza kuondolewa au kupunguzwa kwa kutumia joto kutoka kwa jua kufika kiwango cha 50 ° C ambalo linaweza kuua wadudu.
Andaa jamvi kwa kutandaza nyenzo kama vile majani makavu na mabua kwenye sakafu ili kuzuia upotezaji wa joto. Funika jamvi kwa damani ya plastiki nyeusi ili kunasa joto kutoka kwa jua. Tandaza takriban kilo 5 za mbaazi kwa kila mita mraba kwenye damani ya plastiki nyeusi huku ukiacha nafasi kati ya mbegu. Kisha funika mbegu kwa damani ya plastiki inayopenyeza mwanga wa jua. Kunja kingo za damani ya plastiki na uziimarishe kwa sakafu ukitumia mawe.
Acha mbegu kwenye jua kwa takaribani masaa 2. Hii huua wadudu ikiwa waliomu. Hifadhi mbegu kwenye chombo kisichopitisha hewa. Mbegu hizi zinaweza kutumiak wakati wowote bila kuweka viuatilifu.