Kuzuia pembe za mnyama kuota ni shughuli nzuri sana kwa wafugaji ambayo inapaswa kuizingatiwa kwa uzalishaji bora wa mifugo, kwani mchakato huo ni rahisi kujifunza.
Kuzuia pembe za ndama kuota ni mchakato wa kuchoma pembe za mnyama mchanga katika hatua yake ya awali. Wanyama wasio na pembe huonyesha manufaa kadhaa; nafasi ndogo huhitajika kwa ufugaji, uwezekano wa wanyama kuumizana hupunguka, usafirishaji wa wanyama huwa rahisi.
Hatua za kuzuia pembe za ndama kuota
Anza kwa kunyoa nywele zilizo karibu na sehemu ambapo pembe zinakoota.
Kisha uweke kwa upole chuma maalum kilichopashwa moto kwenye sehemu ambapo pembe zinakoota kwa sekunde 10 ili kuharibu machipukizi ya pembe.
Fanya tena utaratibu huo huo kwa pembe ya pili.
Tumia mafuta ya vuiavijasumu juu ya jeraha ili kuepuka maambukizi.
Mwishowe fuatilia na kutibu majeraha mara kwa mara ili kuepuka maambukizi.