Ufugaji wa kuku bila vifo ndio biashara yenye faida kubwa. Kabla ya kuwapeleka vifaranga wako shambani, jitayarishe kwanza. Kuwa na idadi sahihi ya vyombo vya kulishia na kunyweshea, pamoja na nyenzo zinazotumika kutengenezea banda la vifaranga.
Kujenga eneo la kutunzia vifaranga
Eneo la kutunzia vifaranga linapaswa kuwa angalau 75cm na 1m kutoka ardhini, kwa hivyo joto pungufu litatumika kwa sababu joto la kutosha litahifadhiwa.
Sambaza maranda ya mbao au maranda kwenye sakafu, tandaza pamba juu ya maranda ya mbao ili kuepuka vifaranga kugusana moja kwa moja na maranda, na kula machujo ya mbao.
Wakati wa kushughulikia vifaranga, tumia vyombo vya kunyweshea vinavyofaa ili kuzuia vifaranga kulowa maji wakati wa kunywa, ambayo husababisha nimonia.
Kulisha vifaranga
Wakati wa kuwapa maji, changanya maji na vitamini kwanza, kisha umimine mchanganyiko kwenye chombo cha kunyweshea. Chukua chombo kwenye eneo la kutunzia vifaranga. Paka mafuta ya taa kwenye pande za chombo cha kunyweshea. Usichanganye maji, vitamini na mafuta ya taa.
Taa la umeme linapaswa kuwa chini vya kutosha, na kutoa mwanga wa kutosha. Usitumie taa linalotoa mwanga mwingi sana ili kuepuka ghrama kubwa za umeme. Tumia taa zinazazotoa mwanga mdogo, ambazo huwafurahisha vifaranga.
Mwanga mwingi sana husababisha upofu kwa vifaranga.