Ubora na wingi wa mazao ya mboga huamuliwa na mchakato wa kukuza miche kwenye kitalu unaohusishwa na ubora wa mbegu.
Wakulima hupata mavuno kidogo kutokana na kutumia miche iliyo na ubora duni, ambayo huathiri mahitaji na uuzaji wa bidhaa sokoni.
Uzalishaji wa miche
Ili kukuza miche bora, tumia mbegu zilizoidhinishwa , zisizo na magonjwa, na zinazoota sawasawa. Panda mbegu kwenye viriba. Weka mbegu 1 kwa kila kichanja, kwa kina cha sm 1 na kisha funika na mchanganyiko wa udongo. Maji na hewa ni muhimu kwa ukuaji wa miche. Epuka kusindilia mchanganyiko wa udongo.
Baada ya kupanda, weka chombo cha kuoteshea kwenye meza ya chuma iliyoinuliwa. Epuka kutumia meza za mbao pamoja na kuweka miche chini ili kuzuia magonjwa yanayotokana na udongo.
Nyunyizia maji ili kuhimiza uotaji, na kisha weka mboji ya maji katika wiki 2 hadi 3 na baadaye. Tolea miche kivuli na joto la nyuzi 20–25 za centigrade kwa uotaji sahihi.
Ikiwa miche imekuzwa chini ya damani za plastiki, hakikisha kwamba ziko safi na sio chini ya kivuli ili kuruhusu mwanga wa jua kupenya. Tumia viuatilifu vya kimfumo ili kuzuia wadudu na magonjwa yanayoenezwa na udongo.
Kupandikiza miche
Hatimaye, kupandikiza miche hufanyika kwa wiki 4 na kabla, weka miche chini ya jua moja kwa moja ili kuipa nguvu ya ziada.