Mboga ni mazao muhimu kwa lishe bora. Bustani za mboga zinapaswa kujengwa mahali palipo na jua, mbali na miti mikubwa pamoja na vichaka ili kupunguza ushindani wa virutubisho.
Iwapo unandaa bustani ya mboga, usitumie jembe la tila kwa kuwa linaweza kukata nyasi ambazo huchipuka baadaye na kuwa ngumu kuondolewa. Udongo wa bustani ya mboga unapaswa kuwa unene wa futi 1 – 2 . Kwa hivyo kadiri unavyopanda mboga ndivyo unene na ubora wa bustani utakuwayo.
Hatua
Kata nyasi, geuza udongo na uondoe nyasi na mizizi.
Tenganisha nyasi kutoka kwa udongo ukitumia reki
Jenga kingo za bustani na matofali ili kutenganisha bustani kutoka kwa nyasi na mizizi.
Inua mifuko ya bustani ili maji yasitiririke kwenye bustani.
Weka udongo wa mboji ulio na unene wa futi 1 kwa wakulima wa kilimo-hai.
Ongeza mabaki ya mimea na kuichanganya na udongo, tandaza bustani na ongeza mboji kwenye udongo.