Kiduha hushambulia mimea wakati wa msimu na hata katika msimu unaofuata. Kwa hivyo, unafaa kujua jinsi ya kulinda mpunga dhidi ya shambulio la kiduha.
Kiduha ni magugu mnyonyaji, ambayo ni hatari kwa mpunga, mahindi na mazao mengine ya nafaka. Kiduha hushambulia mizizi ya mazao na kunyonya maji na virutubisho. Kwa hivyo, mimea huathiriwa na magonjwa. Kiduha hutoa mbegu kadha, ambazo kwamba zinaweza kuchanganyika chini ya mchanga.
Usimamizi wa kiduha katika mpunga
Unapovuna mpunga tena, panda tu mchele ndani ya mashimo bila ya kuilima shamba. Hapo, kunde hukaa ardhini na kulinda mimea ya mpunga. Vuna mapema kwa sababu wakati huo kuna magugu kidogo. Kunde pia huzuia mwangaza wa jua nakadhalika, husitisha magugu kukua.
Ili kudhibiti mpunga dhidi ya kiduha , basi usipande mpunga kwenye shamba moja kila mwaka. Baada ya kuvuna mpunga, panda mahindi na mazao mengine ya jamii ya kunde. Kunde hufunika shamba katika na baada ya msimu, na kwa hivyo kuilinda. Hii husaidia kudhibiti kiduha na kuiboresha au kuinawiri ardhi tena. Jamii ya kunde ambayo kwamba ni bora kwa mseto huu ni: mbaazi, mpupu, karanga, soya, maharagwe, crotalaria au stylosanthes.
Unapovuna mpunga tena, panda tu mchele ndani ya mashimo bila ya kuilima shamba. Hapo, kunde hukaa ardhini na kulinda mimea ya mpunga. Vuna mapema kwa sababu wakati huo kuna magugu kidogo. Kunde pia huzuia mwangaza wa jua na kwa hivyo, husitisha magugu kukua.
Mbolea za madini husaidia mazao kukua na kunawiri. Mbinu bora ni kuchanganya aina mbili za mbolea pamoja. Mchanganyiko kuo hutoa virutubisho vinavyohitajika kwa njia iliyokolea na yenye usawa. Unaweza kutumia mbolea ya misombo kama vile NPK na DAP, au mbolea za kimoja kama vile TSP na urea. ukiongeza mboji au samadi pia, hapo basi unahitaji mbolea kidogo ya madini. Mbolea huleta nyenzo za kikaboni kwenye mpunga na kwa hivyo husaidia kuifanya iwe na unyevu na rutuba.
Aina nyingine za mpunga hupinga dhidi ya kiduha. NERICA 2,3,4,8, na 10 ndio sugu zaidi. NERICA 5,9,10 ni wastani. Unaweza kujaribu aina mpya ili ujuwe ni ipi unayopendelea.