Malenge yana maisha mafupi yasipohifadhiwa vizuri. Walakin, maisha yao yanaweza kuongezwa kwa miezi 6 hadi 12 ambayo huhimiza uzalishaji unaoendelea.
Maboga yana virutibusho na yanaweza kudumu kwa muda mrefu ikiwa yamehifadhiwa vizuri. Vuna malenge yaliyokomaa, ambayo yana ngozi ngumu, na hayana kasoro wala wadudu. Kufanya hivyo husaidi malenge kudumu kwa muda kadhaa. Nakadhalika, ondoa uchafu na mabua ili kuepuka kuharibu wengine wakati wa kuhifadhi. Kausha malenge kwa jua kwa muda wa siku 7, na uyafunike kwa damani ya plastiki wakati wa usiku ili kuzuia unyevu na uchafu kuingia.
Kuhifadhi ndani
Andaa chumba cha kuhifadhia, ambacho kinafaa kuwa kavu, poa na kinapenyeza hewa vizuri. Kuhifadhi kwenye sakafu kunahimiza unyevu ambao huharibu malenge. Hifadhi malenge makubwa chini ya madogo kwenye rafu ili makubwa yasidhuru madogo. Dumisha usafi na hahikisha kwamba panya hawaingii chumbani. Kausha malenge juani kwa masaa 1–2 kila wiki wakati wa kuhifadhi. Ondoa malenge yaliyoharibiwa kutoka chumbani na uweke chokaa kwenye nyufa ili kuzuia uharibifu zaidi. Peleka malenge sokoni kwa wingi, kwani hii hupunguza gharama za usafirishaji.