»Kukamua ng‘ombe kwa mkono«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/hand-milking-dairy-cows

Muda: 

00:09:26
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Egerton University

Ufugaji wa ng’ombe kwa maziwa ni chanzo cha chakula na mapato kwa wakulima. Wakati wa kukamua, ni muhimu kudumisha usafi wa kibinafsi na vyombo vyote vinavyotumika.

Iwapo mnyama yuko kwa matibabu, maziwa hayafai kutumiwa hadi kipindi kadhaa. Angalia maagizo kuhusu dawa au wasiliana na daktari wa mifugo ili kuepuka ambukizo.

Mchakato wa Kukamua

Daima usibadilishe nyakati za kukamua ili kupata maziwa zaidi. Dumisha usafi na kufunika kichwa chako ili kuepusha uchafu au nywele kudondoka kwenye maziwa. Baada ya kukamua, safisha vyombo na maji joto na dawa ya kuua viini.

Ng‘ombe anafaa kupumzika, na kulishwa mchanganyiko mzuri wa lishe au lishe la maziwa. Osha na kufuta kiwele cha ng‘ombe ukitumia maji ya vuguvugu na nguo safi ili kuhimiza maziwa yashuke. Tumia mafuta ya kukamua kulainisha matiti.

Maziwa yanafaa kuchunguzwa kwa rangi isiyo ya kawaida au kuganda. Ng‘ombe walioathiriwa wanafaa kukamuliwa mwisho ili kuepusha kuenea kwa maambukizo. Kwa matumizi ya nyumbani unaweza kuchemsha na kuchachawa maziwa kutoka kwa ng‘ombe aliyeathiriwa. Maziwa machache ya kwanza kukamuliwa hayafai kuchanganywa na maziwa mengine kwa sababu ya kiwango kikubwa cha bakteria kilichomu.

Mkao wa Kukamua

Unafaa kuchuchuma katika nafasi ambayo inakuruhusu kutoka wakati ng‘ombe yuko sugu. Weka ndoo ya kukamua chini ya kiwele, akitumia mikono miwili kukamua maziwa na uchague matiti yenye ulalo. Msingi wa titi unafaa kukamuliwa kwa upole ili maziwa yasirudie tena kwenye kiwele. Ng‘ombe anafaa kukamuliwa kabisa ili kuzuia uvimbe wa kiwele. Matiti yanafa kuwekwa katika dawa ya kuua viini au mafuta ya kukamua ili kuzuia maambukizo. Pima na kuandika kiwango cha maziwa kutoka kwa kila ng‘ombe ili kusajili uzalishaji sahihi wa ng‘ombe. Safirisha maziwa kwa vituo vya kukusanya mara tu bada ya kukamua isipokua una kifaa cha kuburudisha.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:20Ufugaji wa ng’ombe kwa maziwa ni chanzo cha chakula na mapato kwa wakulima
00:2000:36Kutosafisha kiwele cha ng‘ombe, matiti, na vyombo husababisha uharibifu wa maziwa.
00:3600:46Maziwa kutoka kwa wanyama walio kwa matibabu hayafai kutumiwa.
00:4600:55Wasiliana na daktari wa mifugo ikiwa kuna ugonjwa.
00:5501:20Usawa wa wakati wa kukamua husaidia kupata maziwa mengi kutoka kwa ng‘ombe.
01:2001:30Matiti ya ng’ombe yanafaa kuwekwa dawa ya kuua viini kabla na baada ya kukamua.
01:3002:25Osha na kufuta kiwele cha ng‘ombe kabla ya kukamua
02:2503:00Ng‘ombe anafaa kulishwa mchanganyiko mzuri wa lishe au lishe la maziwa.
03:0003:38Chuchuma katika nafasi ambayo inakuruhusu kutoka wakati ng‘ombe yuko sugu
03:3804:20Kagua rangi isiyo ya kawaida na kuganda kwenye maziwa. Ng‘ombe walioathiriwa wanafaa kukamuliwa mwisho
04:2004:40Maziwa machache ya kwanza kukamuliwa hayafai kuchanganywa na maziwa mengine.
04:4006:30Msingi wa titi unafaa kukamuliwa kwa upole ili maziwa yasirudie tena kwenye kiwele.
06:3006:40Pima na kuandika kiwango cha maziwa kutoka kwa kila ng‘ombe
06:4007:05Safirisha maziwa kwa vituo vya kukusanya mara tu baada ya kukamua
07:0507:20Safisha vyombo na dawa ya kuua viini na maji moto.
07:2009:26Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *