»Kitalu cha vitunguu«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/onion-nursery

Muda: 

00:13:00
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Agro-Insight

Kutengeneza kitalu cha vitunguu ni chanzo cha mapato ya juu. Miche ya vitunguu huhitaji uangalifu wa makini dhidi ya jua kali na mvua mkubwa. Kitalu huruhusu kumwagilia maji na kulinda miche.

Tumia udongo wenye afya, ambao hujakuza vitunguu kwa miaka kadha ili kudhibiti magonjwa. Unafaa kuinua kitalu ili kuruhusu maji ya ziada kutiririka, na kudhibiti mizizi ya miche kuoza. Boresha udongo kwa kuongeza kikaboni au mboji kwa ukuaji wa miche, na kuwa sugu dhidi ya magonjwa, na kulegeza udongo.

Kutunza miche

Andaa kitalu kiwe na upana wa mita 1 ili kutunza miche kwa urahisi. Zingira kitalu na mpaka mdogo ili kuhifadhi maji ya mvua au ya umwagiliaji. Ondoa magugu, mawe, na vunjavunja vidonge kwa ukuaji mzuri wa mizizi. Ongeza mbolea oza ili kusaidia mizizi ya vitunguu kukua vizuri.

Sawazisha kitalu ili kuwezesha mbegu kuota vizuri. Nunua mbegu kutoka kwa muuzaji anayeaminika ili kuhakikisha mbegu zinaota vizuri. Tunza mbegu dhidi ya magonjwa kwa mapato ya juu. Acha nafasi ya kutosha (umbali wa 5–10 cm, kina cha 1 cm). Funika mbegu na udongo wembamba, na kisha weka matandazo ili kulinda mbegu wakati wa kuota na kuweka udongo unyevu.

Kinga kitalu dhidi ya wanyama wa porini na wa nyumbani. Mwagilia maji kila asubuhi ili mimea isiharibike na kunyauke. Ondoa matandazo baada ya mbegu kuota. Hii husaidia kudhibiti miche kurefuka sana. Palilia kitalu ili kupunguza ushindani wa mimea. Mwishowe, baada ya wiki 3 ongeza mbojea ya madini au mbolea oza kati ya mistari ya mimea ili kurutubisha udongo, na kuimarisha miche.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:49Miche ya vitunguu huhitaji uangalifu wa makini dhidi ya jua kali na mvua mkubwa.
00:5001:03Kitalu huruhusu kumwagilia maji na kulinda miche.
01:0401:54Tumia udongo wenye afya kwa kukuza vitunguu.
01:5503:26Boresha udongo kwa kuongeza mbolea ya kikaboni au mboji.
03:2704:04Andaa kitalu kiwe na upana wa mita 1. Zingira kitalu na mpaka mdogo.
04:0504:18Ondoa magugu, mawe, na vunjavunja vidonge
04:1904:38Ongeza mbolea oza
04:3904:54Sawazisha kitalu
04:5506:07Nunua mbegu kutoka kwa muuzaji anayeaminika
06:0808:03Acha nafasi ya kutosha unapotumia mbegu bora.
08:0409:10Funika mbegu na udongo wembamba na kisha weka matandazo.
09:1109:19Kinga kitalu dhidi ya wanyama wa porini na wa nyumbani.
09:2009:44Mwagilia maji kila asubuhi.
09:4510:12Ondoa matandazo baada ya mbegu kuota
10:1310:43Baada ya wiki 3 ongeza mbolea ya madini au mbolea oza kati ya mistari ya mimea.
10:4410:56Pandikiza wakati miche ina majani 2-3.
10:5713:00Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *