Kutumia wanyama na miti hunaboresha rutuba ya udongo, na kwa hivyo huukinga dhidi ya kiduha.
Kiduha ni gugu kimelea ambayo hushambulia mazao ya nafaka na kwa hivyo huharibu mavuno. Utapata kiduha kidogo kwenye udongo ulio na rutuba, kuliko udongo usio na rutuba. Kufunga mifugo shambani au zizini ndiyo njia rahisi ya kupata samadi na mkojo, na kwa hivyo hurutubisha udongo.
Ulinzi wa miti
Kwenye sehemu zilizo na miti, kuna upepo mdogo na mchanga huwa unyevu. Kwa hivyo ni vizuri kupanda miti shambani. Faida nyingine ni kwamba, wanyama wanapokula majani ya mikayakaya na miti mingine, hunona na kutoa maziwa zaidi, kwa hivyo wanazaa ndama wenye afya.
Samadi ya wanyama
Kila samadi ni nzuri kwa udongo. Haijalishi ikiwa inatoka kwa kuku, mbuzi, kondoo, ngamia au ng‘ombe. Ili kuboresha udongo, unafaa kufungia wanyama wako shambani usiku. Ukiona ukusanyaji wa samadi kwa sehemu moja, unaweza kuisambaza shambani. Tandika zizini kwa kutumia mashina na mabaki ya mimea mingine kavu, ili kunyonya mkojo. Funga mbuzi na kondoo ndani ya kibanda kilichoinuliwa, ambapo ni rahisi kukusanya mkojo na samadi. Njia nyingine nzuri ya kukusanya samadi ni kutumia kibanda cha kuku.
Wakati wa kiangazi, wakulima wengine huomba wafugaji waruhusu ng‘ombe zao shambani mwao. Kwa hivyo, unafaa kuchimba visima au kutunza miti ili kuvutia mifugo shambani mwako wakati wa kiangazi.
Samadi mbichi ina mbegu za magugu. Chimba shimo ili kuhifadhi samadi huko wakati wa mvua. Ikinyesha, mbegu zitaoza. Baadaye, unaweza kutumia samadi shambani.
Epuka kulisha wanyama wako kiduha, kwa sababu samadi yao itasambaza mbegu za kiduha. Zaidi ya hayo, ngoa kiduha kwa mkono hata baada ya kuvuna.