»Kutengeneza mbolea oza ili kushinda kiduha / gugu chawi.«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/node/3229

Muda: 

00:10:14
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Agro-Insight, AMEDD, Countrywise Communication, FLASH, Fuma Gaskiya, ICRISAT, INRAN, UACT

Ni humimu kuhifadhi udongo kuwa na unyevu pamoja na rutuba ili kudhibiti kiduha, kwa sababu kiduha hupenda ardhi ambayo haina rutuba. Mbinu bora, na rahisi ya kuboresha rutuba na kuzuia kiduha ni tugengeneza mbolea oza.

Mbolea ya dukani na mbolea ya kikaboni hudhibiti kiduha ila mbolea za dukani iko ghali. Mbolea oza ni bora kuliko samadi mbichi, kwasababu samadi mbichi yaweza kuchoma mimea hasa kwa udongo wa changarawi. Pia, samadi mbichi huwa na mbegu za magugu. Kwa hivyo, mbolea oza huboresha mpangilio wa mchanga na kuhifadhi udongo ubaki na unyevu kwa mda mrefu.

Kutengeneza mbolea oza

Mbolea oza hutengenezwa kutoka kwa mashina ya nafaka, majani yaliodondoka, mabaki ya nyumbani, samadi ya wanyama na maji. Katika nchi za unyevu, ama wakati wa mvua, mbolea oza hurundikwa ili kiuzuia kulowa. Lakini katika nchi kame, mbolea oza hutengenezwa shimoni ili kuhifadhi unyevu na madani.

Shimo la mbolea oza lina urefu wa mita 4, upana wa mita 2 na kina cha mita moja unusu itakayompa mbolea kutosha hekta moja. Ongeza unyasi, majani yaliodondoka, mashina ya mtama au mawele. Ili kurahisisha mashina kuoza, unaweza kuyakatakata ama uache wanyama wayakanyage na kuyakojolea.

Ongeza takataka ya jikoni na samadi ya wanyama. Kisha ongeza jivu. Mwagilia maji baada ya kila tandiko. Shimo likijaa, lifunike kwa mchanga mwembamba, matawi ya mnazi au jamvi mzee ili kuhifadhi unyevu. Mwagilia maji mbolea ikikauka . Baada ya mwyezi miwili au mitatu, mbolea itakuwa tayari.

Applying compost

Chanaganya mbolea kwa udongo shambani na upande mimea siku hiyo. Mbolea oza yaweza kutumika kabla ya kupanda kwa shimo ndogo au mitaro.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:58Mbolea ya dukani na mbolea ya kikaboni hudhibiti kiduha
00:5901:36Mbolea oza huboresha mpangilio wa mchanga na kuhifadhi udongo ubaki na unyevu kwa mda mrefu.
01:3702:46Samadi mbichi yaweza kuchoma mimea hasa kwa udongo wa changarawi
02:4703:40Mbolea oza hutengenezwa kutoka kwa mashina ya nafaka, majani yaliodondoka, mabaki ya nyumbani, samadi ya wanyama na maji. Mbolea huhitaji maji
03:4104:44Mbolea oza hurundikwa au hutengenezwa shimoni
04:4505:48Shimo la mbolea oza lina urefu wa mita 4, upana wa mita 2 na kina cha mita moja unusu itakayompa mbolea kutosha hekta moja.
05:4906:19Ongeza unyasi, majani yaliodondoka, mashina ya mtama au mawele
06:2006:28Mwagilia maji kila tandiko
06:2907:53Ongeza samadi ya wanyama, na kuku, na jivu.
07:5408:45Baada ya mwyezi miwili au mitatu, mbolea itakuwa tayari.
08:4609:20Mbolea oza yaweza kutumika kabla ya kupanda kwa shimo ndogo au mitaro.
09:2110:14muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *