Kiduha au gugu chawi ni magugu hatari hasa kwa nafaka. Kiduha huharibu shamba pamoja na mavuno. Kwa hivyo, ni muhimu kujua jinsi ya kudhibiti kiduha.
Magugu hunyanganyia mimea mwangaza, maji na virutubisho. Kiduha ni moja wapo ya magugu hatari kwa mtama, mawele na mahindi. Aina moja ya kiduha hutambuliwa kwa maua mekundu ambayo hupatikana Afrika mashariki na kusini . Lile lenye mauma ya zambarau limesambaa barani Afrika kwote. Aina zote mbili zina tabia sawa.
Maisha ya kiduha/ gugu chawi
Kiduha ni magugu vimelea amabayo hufyonza maji na virutubisho kwenye nafaka na hupenda sana kukua kwenye udongo usio na rutuba. Gugu hilo halizai kupitia mizizi, bali kwa mbegu. Kiduha kimoja kinaweza kuzaa laki kadha ya mbegu. Mbegu hizi ni ndogo sana, na wakulima wengi hawawezi kuzitambua. Mbegu za kiduha huonekana kama vumbi nyeusi katika punje ambazo hufanana fukuzi.
Kwa mda wa wiki saba (7), mimea michanga ya kiduha huendelea kukua chini ya ardhi, na hutokea baada ya magugu mengine. Kwa hivyo, mara nyingi kiduha hukosekana katika kupalilia kwa kwanza.
Kutambua kiduha
Unafaa kutambua kiduha kabla haijaanza kutoa maua. Ukiacha kiduha likatoa mbegu nyingi, Lazima ujaribu kulidhibiti mpaka mwaka ujao. Tofauti na magugu mengine, kiduha huonekana kama kwenye fungu kwa shina la mtama, kwa sababu kiduha hushikilia mizizi ya mtama.
Kiduha hushambulii mimea yote, kwamfano “mimea mitego“ kama vile pamba, ufuta, karanga, ugoro, mbaazi, huzuia kiduha. kiduha hushindwa kuingia katikia mizizi ya mimea hiyo ili kufyonza chakula na virutubisho, na mwisho kufa.
Kufanya kazi pamoja
Magugu yanaweza kupitishwa na upepo, maji, mifugo na mazao yaliovamiwa. Ikiwa majirani wako hawadhibiti magugu, utapata shida kubwa miaka ijao. Kwa hivyo, ni muhimu kufanya kazi kwa pamoja na majirani ili kudhibiti kuduha.